Empowering Youth and Women Groups for Sustainable Agriculture (AID-I) in the Regions of Mbeya, Songwe & Ruvuma

Empowering Youth and Women Groups for Sustainable Agriculture (AID-I) in the Regions of Mbeya, Songwe & Ruvuma

04/04/2024
in News

KUWEZESHA VIKUNDI VYA VIJANA NA WANAWAKE ILI KUCHANGIA UKUAJI WA MFUMO ENDELEVU WA CHAKULA KWA KIZAZI KIPYA (AID-I) MKOA WA MBEYA, SONGWE, NA RUVUMA

Rikolto ni Shirika lisilo la Kiserikali la kimataifa lenye uzoefu wa zaidi ya miaka 40 katika kushirikiana na vyama vya wakulima na wadau wa minyororo ya chakula katika bara la Afrika, Asia, Ulaya, na Amerika ya Kusini. Rikolto inaendesha programu katika nchi 17 ulimwenguni kote kupitia ofisi saba za kikanda. Rikolto ina nia kubwa ya kukabiliana na moja ya changamoto kubwa tunazokabiliana nayo - kuhakikisha kuwa tunayo mifumo ya chakula inayotoa suluhisho kwa sisi sote hapo baadaye na ambayo haiilemei sayari yetu zaidi ya uwezo wake. Kwa hiyo, tunajiuliza swali: "Tutakula nini kesho?"

Rikolto kupitia ushirikiano wa RUSOMBE pamoja na washirika wengine wa utekelezaji (BRITEN na Rotai) kupitia ufadhili kutoka AGGRA wanatekeleza programu iliyoitwa "Kuongeza Kasi ya Kufikisha Ubunifu" kwa lengo la kuongeza upatikanaji wa pembejeo bora na masoko nchini Tanzania, kwa kuzingatia mikoa ya Mbeya, Songwe na Ruvuma. Mchango kwa Rikolto unalenga kuongeza ushawishi wa teknolojia za kilimo ili kuongeza uzalishaji endelevu wa mazao muhimu (Mboga, Mahindi, Soya, Mpunga na Maharage) kupitia mbinu inayoongozwa na soko.

Pia kupitia AID -I Programe tunalenga kuwawezesha vijana na wanawake wenye umri wa miaka kati ya 15-29, kuimarisha mifumo ya chakula na lishe Kutoka mikoa ya Mbeya, Ruvuma na Songwe. Vijana hawa wawe wanajishughulisha Shughuli za kilimo na ubunifu kwenye kilimo hasa katika mnyororo wa thamani wa mazao ya Mpunga, mahindi, maharage, soya na kilimo cha mazao ya bustani.

Hivyo mradi unalenga kuwawezesha vikundi vya ujasiliamali na kilimo vya vijana wa kike na wakiume kwa kuendeleza ubunifu na Biashara.Mradi unalenga Vikundi e vinavyojihusisha na kilimo biashara kwenye mnyororo wa thamani wa Mpunga, mahindi , soya na kilimo bustan ambapo vikundi hivi vitaongezewa elimu na ujuzi kwenye biashara , usimamizi wa biashara na kisha wataungalishwa na wadau mbalimbali wanaotoa huduma za kifedha, makampuni yanayosambaza technolojia mbali mbali za kilimo, masoko yenye tija, ushauri wa kibiashara, na watoa huduma za zana za kilimo.

Vigezo vya kushiriki

Ili vijana waweze kuchaguliwa kushiriki katika mradi huu wanapaswa kuwa na vigezo vifuatavyo:

  • Wawe vijana ambao wako kwenye kikundi
  • Wawe vijana wenye umri kati ya miaka 15-29 au kikundi cha wanawake pekee
  • Wawe ni wawakaazi wa mkoa wa Mbeya, Songwe au Ruvuma
  • Vijana wawe wanaweza kutenga muda na kushiriki kikamilifu kwenye mradi wa AID-I
  • Wawe na wazo zuri la kuanzisha au kuendeleza kilimo biashara ambalo litatoa huduma kwenye mnyoro wa thamani wa mahindi, maharage, soya na kilimo cha bustani,
  • Waweze kuonesha kwamba wataweza kutengeneza ajira kwa vijana wa kike na wakiume
  • Wazo na biashara yao iweze kuwaunganisha wakulima na masoko yenye tija
  • Wawe na wazo ambalo linalengakuongeza thamani ya mazao,
  • Kuchangia kwenye ukuaji na matumizi ya teckinologia za kidigitali
  • Kuzingatia kuendeleza teachnologia ambazo zitapunguza kuchangia kwa mabadiliko ya tabia ya nchi au athali zitokanazo na mabadilko ya tabia ya nchi ili kumjengea Mkulima mdogo ustahimilivu na kuchochea ukuaji wa mifumo endelevu a chakula.

Muda wa Mwisho wa Maombi

Usipoteze fursa hii ya kipekee! Tuma maombi yako sasa na ujiunge nasi katika kuleta mabadiliko chanya kwenye kilimo na lishe kwenye mikoa tajwa hapo juu. Maombi yatumwe kwa barua pepe eastafrica.recruitment [at] rikolto.org yakiwa na kichwa cha habari “KUWEZESHA VIKUNDI VYA VIJANA NA WANAWAKE” kabla ya tarehe 28 Aprili 2024 saa 5:59 usiku.

Taarifa kuhusu washiriki waliochaguliwa, zitatolewa baada ya kipindi cha wiki 1 mara baada ya kufungwa kwa Tarehe ya kupokea maombi ya usaili.