[ENGLISH VERSION BELOW]
Mwito wa usaili kushiriki mradi wa Vijana na Wanawake wa Generation Food Accelerator
Je, wewe ni mjasiriamali kijana na mwenye shauku ya kuunda suluhisho jipya na bunifu ili kuhakikisha uendelevu na ujumuishaji katika mfumo wa chakula katika Nyanda za Juu Kusini mwa Tanzania? Una biashara au unatarajia kuanzisha biashara katika sekta ya matunda na mboga? Wewe ni mkulima mwenye msukumo, mtoa huduma mwenye maono, mtendaji kazi mbunifu, au labda wewe ni mpishi unayependa lishe?
Jisajili sasa kwa mradi wa Generation Food Accelerator! Tunatafuta wafanyabiashara mbalimbali wanaojihusisha haswa katika mnyororo wa thamani wa kilimo cha matunda na mboga, kwani uwezekano wa kuchangia mfumo endelevu wa chakula unaojumuisha watu wote, hauna kikomo.
Programu inahusika na nini?
Generation Food Accelerator ni mradi unaosimamiwa na kuendeshwa na shirika la Rikolto Africa Mashariki kwa kushirikiana na Sahara Ventures, kupitia ufadhili wa Umoja wa Nchi za Ulaya, chini ya programu kubwa ya AGRI-CONNECT.
Generation Food Accelerator ni mradi uliojikita katika kuibua na kuboresha biashara bunifu zinazolenga mnyororo wa thamani wa mifumo ya chakula kutoka mikoa ya Nyanda za Juu Kusini hususani: Iringa, Njombe, Mbeya, Songwe and Katavi. Mradi huu unajikita katika kutambua vijana wajasiriamali na wengineo wenye mawazo bunifu ya kibiashara yanayoweza kuendeleza na kukuza usawa wa mnyororo wa thamani wa mifumo ya chakula katika Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini,Tanzania.
Mradi unatarajia kusaili biashara mia moja (100), biashara ishirini (20) kila moja kutoka mikoa mitano (5) ya Nyanda za Juu Kusini (Iringa, Njombe, Mbeya, Songwe, and Katavi) kuwa wanufaikaji wa mradi huu. Katika mradi huu, washiriki watapata mafunzo ya kina kuhusu: urasimishaji wa bashara zao, ubunifu wa mtindo wa biashara, chapa na alama za biashara pamoja na utafutahi masoko, masuala ya kodi na kisheria kuhusiana na biashara zao, na nafasi ya kukutana na wajasiriamali waliofanikiwa katika sekta yao kwenye mazingira yao.
Mradi unatarajia kusaili vijana wajasiriamali wenye biashara zinalolenga kutatua changamoto zifuatazo;
- Uzalishaji endelevu na salama wa kilimo cha mbogamboga na kilimo cha mijini(mf. kanuni bora za kilimo, matumizi sahihi ya dawa za kuua wadudu, vifaa vya umwagiliaji kwa kutumia jua, teknolojia bunifu, kilimo cha mboga zilizosahaulika na matunda yenye kiwango cha juu cha virutubisho)
- Utunzaji endelevu na bunifu, ufungaji, usambazaji, usindikaji na kupunguza uaribifu wa mazao ya mbogamboga kwenye mnyororo wote wa thamani baada ya mavuno. (mf.majokofu ya kwenye masoko, Usindikaji wa juisi/supu kutoka uzalishaji wa hali ya chini, usaifir wa umeme, Mboji)
- Utoaji endelevu na jumuishi wa vyakula, kuhakikisha vyakula vyenye afya na lishe vinapatikana kwa watu wote. (mf. Migahawa yenye chakul safi na bora, Utoaji wa lishe bora mashuleni)