Rikolto in Tanzania, in partnership with TCCIA and 360 Connect, invites youth and community groups to participate in the Call for Youth and Community Innovation to promote sustainable landscape management in the Rungwe, Kyela, and Busokelo districts. The project focuses on enhancing climate-smart agriculture, water management, and natural resource conservation. Interested youth and community groups are encouraged to fill out and submit the application form to eastafrica@rikolto.org by October 24th, 2024.
Deadline:
Terms of Reference (ToR) for Call for Community and Youth Innovation in shaping sourcing landscape in Rungwe, Kyela, Mbarali and Busokelo District
1. Introduction
The Sourcing Landscape Management project, implemented by Rikolto in partnership with TCCIA and 360 Connect, is an initiative dedicated to fostering sustainable landscape management and development. This project is strategically implemented across the Rungwe, Busokelo, Mbarali and Kyela district councils in the Mbeya region, Tanzania. By addressing critical environmental challenges, the project aims to enhance the resilience of local ecosystems while promoting sustainable agricultural practices. Through a combination of community engagement, capacity building, and the introduction of innovative practices, the project seeks to ensure that the natural resources within these districts are managed in a way that balances economic growth with environmental conservation. The initiative also aims to improve the livelihoods of the local communities by integrating sustainable practices into the horticulture, cocoa and rice value chains. By fostering collaboration among local stakeholders, including farmers, government agencies, and private sector partners, the Sourcing Landscape Management project aspires to create a model of sustainable development that can be replicated across other regions facing similar challenges. The project envisions a future where the landscapes of Rungwe, Busokelo, Mbarali and Kyela are sustainably managed, ensuring the long-term well-being of both the environment and the people who depend on it.
2. Rationale
The Sourcing Landscape Management project addresses the urgent need to tackle the interconnected challenges of environmental degradation, agricultural sustainability, and community livelihoods in the Rungwe, Busokelo, Mbarali, and Kyela district councils of Mbeya region. These areas, rich in biodiversity and fertile lands, are vital for the cultivation of rice, horticultural crops, and cocoa, which are essential to the economic well-being of local communities. However, unsustainable farming practices, deforestation, and climate change have increasingly undermined the resilience of these ecosystems, leading to soil erosion, degradation of soil fertility, encroachment on protected water sources, reduced water availability for agriculture and other ecosystem users, rising greenhouse gas emissions, loss of biodiversity, and a decline in agricultural productivity.
In response to these challenges, the project aims to promote sustainable landscape management to restore and protect the environment while enhancing agricultural productivity and strengthening the economic resilience of local communities. By integrating sustainable practices into the horticulture, cocoa, and rice value chains, the project adopts a holistic approach that balances environmental conservation with economic growth.
3. Call for Community and Youth innovation for management of sourcing landscape
This call for innovation seeks to identify and support community and youth-led initiatives that can contribute to the project's objectives by promoting sustainable practices among horticulture, cocoa, rice farmers and management of natural resource in Rungwe District, Mbarali, Busokelo Council and Kyela Districts.
4. Objectives
The main objective of this call for innovation is to engage youth in Rungwe, Busokelo,Mbarali and Kyela districts in developing innovative solutions that address the challenges of sustainable landscape management. The call seeks to:
5. Scope of Work
5.1 Targeted Innovations
Community and Youth-led initiatives should focus on the following key areas:
5.2. Target Groups
6. Expected Outcomes
7. Eligibility Criteria
Community led group/Cooperative/Association involved in farming and management of natural resource
8. Application Process
Interested youth innovators are invited to fill and submit the application form
9. Selection Criteria
Proposals will be evaluated based on:
9. Application Pipeline
TANGAZO
Ubunifu kwa Vijana, Vikundi vya Kijamii vyenye mawazo bunifu katika uwekezaji na kuhamasisha utunzaji wa Mazingira kwa Wilaya za Rungwe, Kyela na Busokelo
1. Utangulizi
Mradi wa USIMAMIZI JUMUISHI WA MAZINGIRA KWA USTAHIMILIVU WA HALI YA HEWA MAENEO YA UZALISHAJI unatekelezwa na Rikolto kwa ushirikiano na TCCIA na 360 Connect ni mpango wa kuhamasisha usimamizi endelevu wa mazingira na maendeleo. Mradi huu unatekelezwa kimkakati katika halmashauri za wilaya za Rungwe, Busokelo, Mbalali na Kyela mkoani Mbeya, Tanzania. Kwa kushughulikia changamoto muhimu za mazingira, mradi unalenga kuongeza uhimilivu wa mifumo ya ikolojia huku ukikuza kilimo endelevu. Kupitia ushirikishwaji wa jamii, kuwajengea uwezo, na kuanzisha mbinu za ubunifu, mradi unalenga kuhakikisha rasilimali za asili ndani ya wilaya hizi zinasimamiwa kwa njia inayowianisha ukuaji wa kiuchumi na uhifadhi wa mazingira. Mpango huu pia unalenga kuboresha maisha ya jamii za wakazi wa Rungwe, Busokelo, Mbarali na Kyela kwa kuingiza mbinu endelevu kwenye minyororo ya thamani ya mazao ya mboga na matunda, kakao, na mpunga. Kwa kuimarisha ushirikiano kati ya wadau, ikiwa ni pamoja na wakulima, mashirika ya serikali, na washirika wa sekta binafsi, mradi unakusudia kuhamasisha maendeleo endelevu ambayo yanaweza kuigwa katika maeneo mengine yanayokabiliwa na changamoto zinazofanana na Wilaya hizi. Mradi huu unatarajia pia kuwa wilaya hizi zitahakikisha ustawi wa muda mrefu wa mazingira na jamii husika.
2. Sababu za Kuanzisha Mradi
Mradi huu unachangia hitaji la haraka la kushughulikia changamoto zinazohusiana za uharibifu wa mazingira, uendelevu wa kilimo, na maisha ya jamii katika halmashauri za wilaya za Rungwe, Busokelo, Mbarali na Kyela mkoani Mbeya. Maeneo haya yana sifa ya bayoanuwai tajiri na ardhi yenye rutuba kwa uzalishaji wa mazao ya mpunga, mboga na matunda pamoja na kakao ambayo ni muhimu kwa ustawi wa kiuchumi wa jamii za wenyeji. Hata hivyo, mbinu zisizo endelevu za kilimo, ukataji miti hovyo, na mabadiliko ya hali ya hewa zimezidi kutishia uhimilivu wa mifumo hii ya ikolojia, na kusababisha kukosekana kwa rutuba ya udongo kutokana na mmomonyoko wa udongo, uvamizi wa maeneo yaliyohifadhiwa kama vyanzo vya maji ambayo inasababisha kupungua kwa upatikanaji wa maji kwa ajili ya kilimo na matumizi ya viumbe vingine, kuongezeka kwa halijoto duniani kutokana na ongezeko la gesijoto (greenhouse gas), kupotea kwa bayoanuwai, na kupungua kwa uzalishaji wa kilimo.
Kutokana na changamoto hizi, mradi unalenga kukuza usimamizi endelevu wa mazingira kama njia ya kurejesha na kulinda mazingira ya asili huku ukiongeza uzalishaji wa kilimo na uhimilivu wa kiuchumi wa wananchi wa wilaya hizi. Kwa kuingiza mbinu endelevu kwenye minyororo ya thamani wa mazao ya mboga na matunda, kakao, na mpunga, mradi unalenga kuunda njia jumuishi inayosawazisha uhifadhi wa mazingira na ukuaji wa kiuchumi
3. Wito wa Ubunifu kwa Jamii na Vijana katika uwekezaji na kuhamasisha utunzaji wa mazingira
Wito huu wa ubunifu unalenga kutambua na kusaidia miradi inayoongozwa na jamii na vijana ambayo inaweza kuchangia malengo ya mradi kwa kuhamasisha mbinu endelevu miongoni mwa wakulima wa mazao ya mboga na matunda, kakao, na mpunga na usimamizi wa rasilimali asili katika Wilaya za Rungwe, Busokelo,Mabali na Kyela.
4. Malengo
Lengo kuu la mwito huu wa ubunifu ni kuhusisha vijana na jamii katika wilaya za Rungwe, Busokelo, Mbarali na Kyela katika kuendeleza suluhisho za ubunifu zinazoshughulikia changamoto za usimamizi endelevu wa mazingira. Wito huu unalenga:
5.1 Ubunifu unaolengwa
Jamii na vijana wanaotarajia kushiriki katika mwito huu wanatakiwa kuzingatia yafuatayo
5.2. Makundi Yanayolengwa
6. Matokeo Yanayotarajiwa
7. Vigezo vya ushiriki
8. Mchakato wa Maombi
Wabunifu vijana na vikundi vya kijamii wanakaribishwa kujaza na kuwasilisha fomu ya maombi.
9. Vigezo vya Kuchaguliwa
Mapendekezo yatatathminiwa kwa kuzingatia misingi ifuatayo:
9. Mchakato wa Maombi