YEFFA (Youth Entrepreneurship for the Future of Food and Agriculture) ni mradi unaolenga kuwawezesha vijana wajasiriamali katika mikoa ya Mbeya, Songwe, Njombe, Rukwa, na Katavi ili kuleta suluhisho bunifu kwa mifumo endelevu ya chakula. Kupitia mafunzo, ushauri, na fursa za uwezeshaji wa kibiashara, YEFFA inasaidia biashara zinazolenga kuongeza thamani katika mnyororo wa alizeti kwa kuboresha uzalishaji, kupunguza upotevu wa mazao, na kuimarisha mifumo ya masoko. Ikiwa unamiliki biashara au una wazo la biashara katika sekta ya kilimo na thamani ya alizeti, jisajili bure kabla ya tarehe 8 Machi 2025 kwa kupakua fomu kisha ijazena kuiwasilisha kwenye halmashauri yako au kwa barua pepe eastafrica@rikolto.org. Kwa maswali au msaada wa kujiandikisha, wasiliana na waratibu wa mradi kupitia simu 0763700814. Usikose fursa hii ya kipekee ya kuimarisha biashara yako na kuchangia mfumo jumuishi wa chakula!
Deadline:
WITO WA USAILI KUSHINDANIA MRADI WA KUWEZESHA UJASIRIAMALI KWA VIJANA KWA MUSTAKABALI WA CHAKULA NA KILIMO (YEFFA):
Je, wewe ni kijana mjasiriamali mwenye shauku yakuleta suluhisho bunifu kwa mifumo endelevu ya usalama wa chakula katika mikoa ya Mbeya, Songwe, Njombe, Rukwa, au Katavi? Je, unamiliki au una wazo la biashara inayoongeza thamani katika mnyororo wa mazao ya kilimo, hususani alizeti?
Fursa yako ni sasa! Jisajili na upate nafasi ya kushiriki katika Mradi wa YEFFA (Youth Entrepreneurship for the Future of Food and Agriculturet). Mradi huu unatafuta vijana wa kike na kiume wenye biashara au mawazo ya biashara zinazohusiana na sekta ya kilimo na mnyororo wa thamani wa zao la Alizeti , kwa lengo la kuwawezeshakibiashara na kuimarisha mifumo jumuishi ya chakula.
Kuhusu Mradi wa YEFFA
Rikolto Tanzania imepata ufadhili kutoka AGRA kutekeleza Mradiwa YEFFA, unaolenga kuimarisha ujasiriamali wa vijana kwa mustakabaliwa Chakula na Kilimo kwa kuwawezesha vijana na wanawake kupitia mnyororojumuishi wa thamani wa alizeti unaoongozwa na soko. Mradi huu unatekelezwakwa kushirikiana na wadau mbalimbali nchini Tanzania na kufadhiliwa na MastercardFoundation.
YEFFA inalenga kufikia wakulima wadogo waalizeti 100,000, wakiwemo vijana na wanawake, na kuwawezesha zaidi ya vijana 12,068 kupata ajira yenye heshima na tija kwenye mnyororo wa thamani waalizeti katika mikoa ya Mbeya, Songwe, Njombe, Rukwa, na Katavi.
Mradi unatarajia kusaili biashara 125 (25 kutokakila mkoa), ambazo zitapata mafunzo na fursa za uwezeshaji wa kibiashara.
YEFFA Inalenga Kuwezesha Biashara Zipi?
Mradi huu unalenga kusaidia biashara zinazoshughulika na:
Mtiririko wa Mradi wa YEFFAMradi utatekelezwa kwa hatua zifuatazo:
1. Usajili na Usaili
2. Mafunzo Kambini
3. Ushauri na Malezi ya Kibiashara
4. Fainali na Uwekezaji
Nani Anaweza Kushiriki?
Usikose nafasi hii ya kipekee! Pakua fomu hapo chini kisha uijaze na uiwasilishe kwenye halmashauri yako au unaweza kutuma kwenye barua pepe: eastafrica@rikolto.org mwisho Tarehe 8 Machi 2025. Endapo kama utakutana na changamoto katika kujiandikisha tafadhali wasiliana na mratibu wa mradi kupitia namba ya simu: 0763700814.