APPLICATION FOR PROJECT ON YOUTH AND WOMEN (NEW GENERATION FOOD ACCELERATOR (AID-I) MBEYA, SONGWE AND RUVUMA REGION

APPLICATION FOR PROJECT ON YOUTH AND WOMEN (NEW GENERATION FOOD ACCELERATOR (AID-I) MBEYA, SONGWE AND RUVUMA REGION

21/03/2024
in News

FOMU YA USAILI MRADI WA VIJANA NA WANAWAKE (NEW GENERATION FOOD ACCELERATOR (AID-I) MIKOA YA MBEYA, SONGWE NA RUVUMA

Mradi huu unasimamiwa na kuendeshwa na shirika la RIKOLTO Afrika Mashariki kwa kushirikiana na wadau wake chini ya ufadhili wa shirika la AGRA. Mradi huu utakaotekelezwa kwa kipindi cha ndani ya mwaka 2024, ni kwa ajili ya kuimarisha mifumo ya chakula na lishe kwa vijana na wanawake waliopo katika mikoa ya Mbeya, Songwe na Ruvuma. Mradi umelenga kuendeleza wabunifu na wajasiriamali na kuboresha mifumo ya kilimo biashara kupitia mnyororo mnyororo wa thamani wa uzalishaji wa mazao ya mpunga, mahindi, maharage, soya, na mazao ya bustani (mbogamboga na matunda) pamoja na mifumo ya chakula na lishe.

Mradi huu unahitaji kuendeleza vijana na wanawake wajasiriamali na wenye biashara zinazoweza kuendeleza, kuchochea na kukuza ama kuchagiza maendeleo ya mifumo bunifu inayolenga kuongeza thamani ikiwa ni pamoja na kutatua changamoto mbalimbali za uhudumiaji wakulima wadogo na wakati, pamoja na kuongeza ubora wa bidhaa kwa walaji wa mwisho na mifumo ya masoko.

Vigezo vya kuweza kushiriki

 • Ili vijana waweze kuchaguliwa kushiriki katika mradi huu wanapaswa kuwa na vigezo vifuatavyo:
 • Uwe kijana mwenye umri kati ya miaka 18-29
 • Uwe ni mkazi wa mkoa wa Mbeya, Songwe au Ruvuma
 • Uwe unaweza kusoma, kuzungumza na kuandika lugha ya kiswahili au kiingereza.
 • Uwe tayari kutenga muda na kushiriki kikamilifu kwenye mradi wa AID-II
 • Uwe na sampuli kifani au biashara bunifu iliyokamilika na inayolenga kutatua changamoto kwenye mnyororo wa thamani wa mbogamboga na matunda au lishe, pamoja na mazao ya mpunga, mahindi, maharage, soya, na kuweza kuthibitisha upatikanaji wa fursa za ajira kwa vijana na wanawake ama kuwashirikisha vijana wengine waishio kwenye mazingira magumu na kuonesha uwezekano wa kukua kwa biashara husika.
 • Uwe na shauku na maono ya kukuza na kuendeleza biashara kwenye mnyororo wa thamani wa mbogamboga na matunda au lishe.

Maelekezo ya kushiriki

 1. Pakua fomu hapo chini na
 2. Tafadhali jibu maswali yote
 3. Zungushia duara au weka tiki katika maswali yasiyo na nafasi ya kujibu
 4. Jibu kwa ufupi na kwa kueleweka
 5. Tuma majibu yako kwenda eastafrica.procurement [at] rikolto.org

Muda wa mwisho kupokea maombi ni tarehe 10 April 2024 Saa 5:59 Usiku. ……………………………………. Taarifa kuhusu washiriki waliochaguliwa, zitatolewa baada ya kipindi cha wiki 1 mara baada ya kufungwa kwa Tarehe ya kupokea maombi ya usaili. …………………………………………

PAKUA FOMU YA USAILI MRADI WA VIJANA NA WANAWAKE HAPO CHINI KISHA IJAZE NA UITUME KWENDA eastafrica.procurement@rikolto.org